Israel yashambulia jengo la Mushtaha mjini Gaza
5 Septemba 2025Matangazo
Shambulio hilo limetokea wakati jeshi la nchi hiyo linapozidisha oparesheni inayolenga kuchukua udhibiti wa mji wa Gaza unaokaliwa na takriban Wapalestina milioni moja.
Kwa mujibu wa jeshi la Israel IDF, jengo hilo lilikuwa likitumika na wapiganaji wa Hamas kwa shughuli za kipelelezi na kupanga mashambulizi.
Picha za setilaiti zimeonyesha uwepo wa idadi kubwa ya mahema yanayohifadhi watu waliokimbia vita karibu na jengo hilo.