Israel yasema vita vya Gaza vitaisha mateka wakiachiwa huru
7 Septemba 2025Matangazo
Matamshi ya Saar wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Jerusalem akiwa na mwenzake wa Denmark, yanakuja siku moja baada ya Hamas kusisitiza msimamo wake wa muda mrefu kwamba itaawacha huru mateka wote wa Israel wanaoshikiliwa Gaza, ikiwa Israeli itakubali kumaliza vita na kuondoa vikosi vyake kutoka Mji wa Gaza.
Katika hatua nyingine, jeshi la Israel limesema makombora mawili yamerushwa leo kutoka ukanda wa Gaza kuelekea Israel huku kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Islamic Jihad likidai kuhusika na shambulizi hilo ambalo halikusababisha hasara au uharibifu wowote.
Katika taarifa, jeshi hilo limesema kuwa kombora moja lilidunguliwa na moja likaanguka kwenye eneo la wazi.