Israel: Tutaishambulia Gaza iwapo mateka hawatoachiliwa
16 Februari 2025Matangazo
Akizungumza na waandishi habari akiwa pamoja na waziri wa nchi za nje wa Marekani Marco Rubio, aliyeko ziarani nchini humo, Netanyahu amesema Marekani na Israel inamkakati mmoja na haziwezi kuizungumzia mikakati hiyo hadharani ikiwa ni pamoja na kulitokomeza kabisa kundi la Hamas.
Marco Rubio pia ameshinikiza kuwa kundi la Hamas haliwezi kuendelea kuiongoza Palestina.
Ziara ya Rubio: Netanyahu asifu msimamo wa Trump kuhusu Gaza
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani anatarajiwa pia kushinikiza pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuuchukua Ukanda wa Gaza na kuwahamisha Wapalestina zaidi ya milioni mbili kutoka kwenye Ukanda huo na kuwapeleka kwenye nchi za Kiarabu.
Netanyahu ameuita mpango huo kama mpango wa kijasiri.