Israel yaahirisha zoezi la kuwaachia wafungwa wa Kipalestina
23 Februari 2025Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema hii leo kwamba zoezi la kuwaachia wafungwa wa Kipalestina chini ya makubaliano ya usitishaji vita Gaza, litacheleweshwa hadi pale kundi la Hamas litakapokomesha kile amekitaja kuwa "hafla za udhalilishaji" wakati linapowaachia mateka wa Israel.
Ofisi ya Netanyahu ilisema kuwa, Hamas imekuwa ikifanya ukiukwaji wa mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na sherehe za kufedhehesha ambazo zinawavunjia heshima mateka. Hapo jana Hamas iliwaachia mateka 6lakini Israel iliahirisha kuwaachilia wafungwa wa Kipalestina.
Hamas imeitaja hatua hiyo kuwa ni ukiukwaji wa wazi wa makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo awamu ya kwanza itakamilika mwezi Machi.
Tangu awamu ya kwanza ya usitishaji mapigano ilipoanza Januari 19, Hamas imewaachia mateka 25 wa Israel walio hai. Israel ilitarajiwa kuwaachia wafungwa zaidi ya 600 wa Kipalestina.