Israel yasema itaanzisha utawala mpya katika Ukanda wa Gaza
24 Machi 2025Serikali ya Israel imethibitisha kwamba itaanzisha idara mpya itakayowashughulikia raia wa Gaza wanaotaka kuondoka kwa hiari kutoka kwenye eneo hilo.Mazungumzo kuhusu amani ya Gaza yafanyika Misri
Msemaji wa waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu, amesema Baraza la Mawaziri la Usalama limeidhinisha pendekezo lililotolewa na waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz la kuanzisha kitengo cha maafisa watakaopewa jukumu la kuandaa mpango wa kuwaondoa kwa hiari, wakazi wa ukanda wa Gaza na kuwapeleka katika mataifa mengine.
Haya yanajiri baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kupendekeza makazi mapya ya Gazayenye idadi ya zaidi wa watu milioni mbili kwenda nchi za Kiarabu ikiwemo Misri.
Mustakabali wa maisha ya raia ya Gaza bado yanasalia mashakani baada ya Israel kuanzisha tena mashambulizi yaliyowaua zaidi ya watu 700 kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza .