MigogoroMashariki ya Kati
Israel yasema imeishambulia hospitali Ukanda wa Gaza
13 Mei 2025Matangazo
Israel imedai shambulizi lake limeilenga hospitali ya Al-Nasser iliyo kwenye mji wa Khan Yunis, ambayo inasema imekuwa ikitumiwa na Hamas kama kamandi ya kupanga na kutekeleza hujuma zake.
Kundi hilo limekanusha madai hayo na kuikosoa Israel kwa kushambulia jengo la upasuaji la hospitali hiyo. Shambulizi hilo ambalo inaarifiwa limemuua mwandishi mmoja wa habari, limehitimisha usitishaji wa mapigano kwa muda ili kuruhusu kuachiwa huru kwa mateka mwenye uraia pacha wa Israel na Marekani.
Raia huyo Edan Alexander aliachiwa hapo jana baada ya kukaa mikononi mwa Hamas tangu alipotekwa nyara Oktoba 7 mwaka 2023 wakati kundi hilo lilipoishambulia Israel.