Israel yaripotiwa kuendeleza mashambulizi kusini mwa Syria
30 Julai 2025Matangazo
Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu la Syria limesema droni za Israel ziliwashambulia wapiganaji wa Kibedui na wanagambo wanaoiunga mkono serikali magharibi mwa Sweida.
Kwa mujibu wa shirika hilo, mashambulizi hayo yalikuwa sehemu ya operesheni pana ya Israel kwenye jimbo hilo la kusini mwa Syria.
Mashahidi wameripoti kiwango kikubwa cha droni na helikopta za Israel kwenye maeneo mbalimbali ya jimbo hilo ndani ya masaa 24 yaliyopita.
Jeshi la Israel halijatowa taarifa yoyote kuhusu mkasa huo. Kiasi cha watu 1,100 wameuawa tangu katikati ya mwezi huu kutokana na mapigano kati ya makundi ya Druze na Mabedui na mashambulizi ya Israel, kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za binaadamu.