MigogoroMashariki ya Kati
Miili ya mateka wawili iliyokuwa Gaza yarudishwa Israel
29 Agosti 2025Matangazo
Kulingana na ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu mwili wa mwanamume huyo umetambuliwa kuwa ni wa Ilan Weiss wa Be'eri. Mwili wa mateka mwingine haujatambuliwa. Mateka 50 kati ya 250 waliochukuliwa na wanamgambo wa Hamas wanaaminika kuwa bado wako Ukanda wa Gaza na 20 wanadhaniwa kuwa bado wako hai. Haya yanajiri huku jeshi la Israel likisema limesitisha mapumziko ya mchana yanayotoa nafasi ya kuwasilishwa kwa misaada katika jiji la Gaza na kudai kuwa eneo hilo ni hatari.
Wakati huohuo Wizara ya Afya ya Gaza imesema idadi ya wakaazi wa ukanda huo waliouawa kutokana na vita kati ya Israel na hamas, sasa imefika zaidi ya watu 63,000.