Israel yaonywa kuhusu mwenendo wake katika Ukanda wa Gaza
20 Mei 2025Viongozi wa Uingreza, Ufaransa na Canada wamelaani vitendo viovu vya Israel katika Ukanda wa Gaza na kuonya kuchukua hatua za pamoja ikiwa haitasitisha mashambulizi ya kijeshi yaliyokithiri katika ardhi ya Palestina.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewakosoa waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na waziri mkuu wa Canada Mark Carney, akisema taarifa yao ya pamoja ya jana Jumatatu ni zawadi kubwa kwa kundi la Hamas katika vita vya Gaza.
Israel kufanya operesheni ya ardhini na kupeleka msaada Gaza
Starmer, Macron na Carney walikosoa hatua ya Israel ya kuzuia misaada isipelekwe Gaza na kauli za mawaziri katika serikali ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ambao wametishia uhamishaji wa Wapalestina.