Israel yaonya kuwa itashambulia eneo lolote nchini Lebanon
29 Machi 2025Netanyahu ametoa kauli hiyo baada ya jeshi la Israel kufanya shambulizi la kwanza kusini mwa Beiruttangu kusitishwa kwa mapigano mwezi Novemba na wanamgambo wa Hezbollah.
Israel ilifanya mashambulizi hayo muda mfupi baada ya jeshi lake kusema limezuwia makombora mawili kutokea Lebanon.
Mapema siku ya Ijumaa jeshi la Israel lilitoa onyo kwa wakaazi likiwataka waondoke haraka katika baadhi ya maeneo yaliyo nje kidogo mwa mji mkuu wa Beirut na kuapa kwamba lingelipa kisasi kutokana na mashambulizi yaliyofanywa kaskazini mwa Israel kutoka Lebanon. Maeneo hayo yaliyoshambuliwa yanafahamika kuwa ngome kuu ya kundi la Hezbollah.
Mwanadiplomasia wa zamani wa Israel aukosoa utawala wa NetanyahuKundi hilo hata hivyo limekanusha kuwa halikuhusika na mashambulizi hayo na limesema Israel inatafuta sababu ya kuendelea kuishambulia Beirut.
Waziri Mkuu wa Lebanon Nawaf Salam ameyaelezea mashambulizi ya Israel kwenye vitongoji vya kusini mwa Beirut kuwa yanahatarisha kuongeza mvutano.
Naye Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amelaani mashambulizi hayo aliyosema "hayakubaliki dhidi ya Beirut". Akizungumza katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na Rais wa Lebanon Joseph Aoun, Macron alisema mvutano huo mpya "unaashiria hatua ya mabadiliko," akiongeza kuwa Ufaransa itaendelea kuwa upande wa Lebanon ili kuisaidia kulinda "uhuru" na usalama wake.
Israel yailaumu Lebanon kwa shambulio la makombora, yajibu mapigo
"Jeshi Israel lazima liondoke haraka katika maeneo matano inayoendelea kuyakalia katika ardhi ya Lebanon ili kuruhusu jeshi la Lebanon kupelekwa huko na raia kurejea nyumbani. Ufaransa itaendelea kutoa mapendekezo okatika mwelekeo huu wa mapendekezo halisi na ya kweli kuhusiana na matarajio ya Lebanon na Israel," alisema Macron.
Juhudi za usitishaji mapigano Gaza
Afisa mmoja mwandamizi wa kundi la wanamgambo la Hamas Bassem Naim, amesema mazungumzo kati ya kundi hilo la Kipalestina na wapatanishi kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano yanashika kasi huku Israel ikiendeleza operesheni kali huko Gaza.
Afisa huyo ambaye ni mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Hamas amesema katika taarifa yake kuwa mazungumzo hayo yanalenga "kupatikana kwa makubaliano ya kusitisha vita, kufunguliwa kwa vivuko na kuruhusu misaada ya kibinadamu."
Soma: Kundi la Hamas limesema liko tayari kwa mazungumzo na Israel
Duru za Kipalestina zilizo karibu na Hamas zimelialeza shirika la habari la AFP kwamba mazungumzo hayo yalianza Alhamisi jioni kati ya kundi la wanamgambo na wapatanishi kutoka Misri na Qatar ili kufufua makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachilia mateka Gaza.
Usitishaji wa mapigano dhaifu ambao ulileta utulivu wa wiki kadhaa katika Ukanda wa Gaza ulimalizika mnamo Machi 18 wakati Israeli iliporejelea kampeni yake ya mashambulizi katika ukanda huo.
Na Umati mkubwa wa watu uliingia mitaani katika miji mikuu ya Iran, Iraq na Yemen siku ya Ijumaa kwa ajili ya maonyesho ya kila mwaka ya kuwaunga mkono Wapalestina na kuipinga Israel.
Maandamano hayo yanayotaka Jerusalem irejeshwe kwa Wapalestina, kwa kawaida hufanyika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Umati wa watu ulikusanyika katika mitaa ya Tehran baada ya kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei kuwataka watu wa Iran kuandamana dhidi ya "hila za maadui"