Israel yalaani shambulio dhidi ya wayahudi Colorado
2 Juni 2025Mwanadiplomasia wa ngazi za juu wa Israel,Gideon Sa'ar, amelaani tukio la jana Jumapili la kushambuliwa huko Colorado, Marekani, waandamanaji waliokuwa na bendera za Israel, wakidai kuachiliwa huru kwa mateka wanaoshikiliwa Gaza.
Waziri huyo wa mambo ya nje waIsraelamedai kwamba tukio hilo limechochewa na vyombo vya habari,akiliita ni tukio baya la kigaidi la chuki dhidi ya wayahudi ambalo limetokana na kile alichokiita, uwongo unaosambazwa na vyombo vya habari.
Mtu mmoja aliyesikika akipaaza sauti akisema, Ikombolewe Palestina, aliwatia moto waandamanaji waliokuwa wamekusanyika kudai mateka Waisrael waachiwe huru Gaza.Wengi waliungua na wengine kujeruhiwa.
Waziri mkuu wa Israel BenjaminNetanyahu amesema anataraji kwamba mamlaka za Marekani zitachukuwa hatua kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria muhusika.