Israel yalaani kuhusishwa na mauaji ya halaiki Gaza
5 Septemba 2025Matangazo
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, Oren Marmorstein, kupitia mtandao wa X amesema "Tunalaani vikali madai yasiyo na msingi yaliyotolewa na Makamu wa Rais Mtendaji wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya." Aidha msemaji huyo aliongeza kwa kusema badalaya kueneza tuhuma hizo zinazotolewa na Hamas, Ribera alipaswa kutoa wito wa kuachiliwa kwa mateka wote na kwa Hamas kuweka silaha chini ili vita viishe. Katika hatua nyingine Jeshi la Israel (IDF) limethibitisha kuwa linaudhibiti wa kijeshi wa asilimia 40 ya Mji wa Gaza, kwa mujibu wa msemaji wake Brigedia Jenerali. Effie Defrin, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Septemba 4, 2025.