Israel yakataa shinikizo la Umoja wa Ulaya kuhusu Gaza
21 Mei 2025Israel imepinga uamuzi wa Umoja wa Ulaya kudurusu upya mkataba wake wa ushirikiano katika juhudi ya kuishinikiza kuhusiana na mashambulizi yake makali katika Ukanda wa Gaza.
Waziri wa mambo ya nje wa Israel asema nchi hiyo ni kiungo muhimu kwa Ulaya
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Israel Oren Marmorstein amesema katika ujumbe aliouandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba wanakataa kabisa muelekeo uliochukuliwa katika taarifa hiyo, ambayo inaonyesha kutokuelewa kabisa ukweli kuhusu hali halisi ambayo Israeli inakabiliana nayo.
Mapema Jumanne, Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas alisema katika taarifa kwamba umoja huo ulikuwa unatafakari kudurusu upya ushirikiano wake na Israel kwa kuzingatia operesheni mpya huko Gaza kufuatia mzingiro wa Israeli uliodumu wiki 11 katika eneo hilo.