Israel yaishinikiza Hamas iwaachie huru mateka wake
31 Mei 2025Matamshi hayo yametolewa na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Israel Katz ambaye amelitaka kundi la Hamas kutia saini rasimu ya mkataba iliyowasilishwa na mjumbe maalum wa Rais Donald Trump wa Marekani Steve Witkoff.
Hamas imeikataa rasimu hiyo ikisema haijakidhi matakwa yake ikiwemo vikosi vya Israel kuondoka kabisa ndani ya ardhi ya Gaza na vita kumalizika.
Rais Trump ameelezea matumaini yake hapo jana akisema "makubaliano yako mbioni kufikiwa" lakini hadi sasa bado hakuna ishara za Hamas kulegeza msimamo wake.
Wakati huo huo Israel imesema haitoshiriki mpango wa kufanikisha ziara inayopangwa na mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi 6 za kiarabu kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi.
Israel imesema ziara hiyo mjini Ramallah, yaliko makao makuu ya Mamlaka ya Palestina ni kitisho kwa usalama wake.