Israel imeshambulia Makao Makuu ya Jeshi la Syria na maeneo karibu na Ikulu mjini Damascus, wakati mapigano kati ya serikali ya Syria na kundi dogo la Wadruze yakiendelea. Baada ya mashambulizi hayo, Marekani imetangaza kuwa pande zote zimekubaliana kuchukua “hatua mahususi” za kusitisha machafuko.