Israel yaishambulia mifumo ya ulinzi ya Syria
11 Machi 2025Mashambulizi hayo yameilenga mifumo ya ulinzi wa anga na maeneo mengine ya kijeshi katika shambulio la hivi karibuni zaidi katika nchi hiyo jirani.
Taarifa ya jeshi hilo la Israel imesema ndege zake za kivita ziliharibu vifaa vya rada vinavyotumika kufanyia uchunguzi wa kijasusi wa anga pamoja na kamandi na maeneo ya kijeshi yenye silaha na zana za kijeshi za utawala wa Syria.
Jeshi hilo limedai kuwa kuwa mashambulizi hayo yalifanyika kuondoa vitisho vya siku zijazo.
Taarifa hiyo pia imesema uwepo kwa vifaa hivyo kusini mwa Syria kunaleta tishio kwa Israeli na shughuli za jeshi la nchi hiyo.
Kwa upande wake, vyombo vya habari vya serikali ya Syria vimesema kuwa Israel ilishambulia mkoa wa kusini wa Daraa, huku shirika moja la kufuatilia vita likiripoti takribani mashambulizi 17 dhidi ya ngome za jeshi la zamani la Syria.