Israel yaipuuza ripoti ya Amnesty kuhusu mauaji ya Gaza
29 Aprili 2025Matangazo
Israel imepuuzilia mbali ripoti ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International kuhusu mauaji ya kiholela katika Ukanda wa Gaza ikiita kuwa uongo usio na msingi.
Shirika hilo limeituhumu Israel leo Jumanne kwa kufanya mauaji ya kiholela dhidi ya Wapalestina huko Gaza kwa kuwaondoa kwa lazima wakaazi na kwa kusababisha janga la kibinadamu kwa makusudi.
Katika ripoti yake ya kila mwaka Amnesty International imesema Israel inachukua hatua kwa dhamira mahususi ya kuwaangamiza Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na hivyo kufanya mauaji ya halaiki.
Israel imekanusha mara kwa mara madai kama hayo kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu na mataifa kadhaa.