Israel yaimarisha mashambulizi baada ya agizo la Netanyahu
11 Agosti 2025Hatua hiyo imejiri muda mfupi baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kutangaza operesheni mpya ya kumaliza vita haraka huko Gaza.
Netanyahu alisema operesheni hiyo mpya italenga Jiji la Gaza, akilitaja kama "mji mkuu wa ugaidi” wa wanamgambo wa Hamas. Aliagiza jeshi kuharakisha mipango ya kuchukua udhibiti wa jiji hilo.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameonya kuwa hatua hiyo inaweza kusababisha kile alichokiita "janga lisilo na kifani,”. Ujerumani tayari ilishatangaza kuwa itasitisha usafirishaji wa silaha za kijeshi kwenda Israel. Uingereza na washirika wengine wa Ulaya waliitaka Israel kufikiria upya hatua hiyo ya kuongeza mashambulizi.
Katika tukio jingine, mazishi ya mwandishi habari wa Aljazeera Anas Al Sharif na waandishi wengine watano waliouawa kwenye mashambulizi ya Israel yamefanyika huko Gaza.
Israel ilithibitisha kumuua Al Sharif ikimtuhumu kuwa kiongozi wa wanamgambo wa Hamas.