Israel yaikosoa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani
14 Aprili 2025Israel imeiokosoa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani kutokana na ujumbe uliowekwa kwenye ukurasa wa mtandao wa X na wizara hiyo, ukihoji mashambulio ya hivi karibuni yaliyofanywa na jeshi la Israel dhidi ya jengo moja la hospitali kaskazini mwa Gaza.
Israel imeikosoa taarifa hiyo ya Ujerumani, ikisema haikuwa na maelezo sahihi.Soma pia: Israel yashambulia hospitali kaskazini mwa Gaza
Wizara ya mambo ya nje ya Israel imekanusha kuishambulia hospitali kwa ujumla, bali kupitia mtandao wa X imesema kwamba shambulio hilo lililenga shabaha jengo moja tu, lililokuwa likitumiwa na wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas, kama kituo cha kuongoza shughuli zao.Soma pia: Gaza: Hospitali iliyoshambuliwa na Israel imeharibiwa vibaya
Taarifa hiyo ya Israel ilikuwa ikijibu ujumbe uliochapishwa Jumapili na ofisi ya waziri wa mambo ya nje anayeondoka, Annalena Baerbock, uliosema ukatili wa Hamas unapaswa kukabiliwa, lakini sheria ya kimataifa ya kibinadamu izingatiwe na hasa kulindwa kwa maeneo ya kiraia.