Israel yaidhinisha utanuzi wa operesheni ya kijeshi Gaza
5 Mei 2025Matangazo
Baraza la mawaziri la usalama nchini Israel limeidhinisha utanuzi wa operesheni ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza ambayo inajumuisha hatua ya kuyatwaa maeneo ya ardhi ya Wapalestina na kuwaondoa wakaazi.Soma pia: Watu 20 wauawa Gaza, Wahouthi waishambulia Israel
Uamuzi huo uliopitishwa usiku wa kuamkia leo, umepitishwa saa chache baada ya jeshi kutangaza mwito wa kutaka maelfu ya wanajeshi wa akiba kutanua operesheni zao dhidi ya kundi la Hamas, katika Ukanda huo wa Gaza.
Hata hivyo kundi la Israel la harakati ya kuwapigania mateka wanaoshikiliwa Gaza, limeukosoa mpango huo wa serikali likisema ni wa kuwatowa muhanga mateka hao na unapaswa kuitwa mpango wa Smotrich na Netanyahu, wa kuwatowa muhanga mateka.