Israel yaidhinisha operesheni mpya ya kijeshi kuitwaa Gaza
5 Mei 2025Israel imeidhinisha mipango ya kulitwaa eneo zima la Ukanda wa Gaza na kuendelea kulishikiliwa kwa muda usiojulikana.
Maafisa wawili wa nchi hiyo waliozungumzia hatua hiyo wamesema baraza la mawaziri la usalama lilipitisha uamuzi huo kupitia mchakato wa kura uliofanyika mapema leo asubuhi.
Yair Lapid kiongozi wa upinzani nchini Israel akizungumzia uamuzi huo amesema hakuna anayefahamu kwa undani mpango huo.Soma pia: Mpango wa Israel kuikalia tena Gaza wapingwa kimataifa
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu amesema operesheni mpya itakuwa kubwa na Wapalestina watahamishwa.
Uongozi wa jeshi la Israel umewaita maelfu ya wanajeshi wa akiba kujiunga na mpango huo mpya, ambao maafisa wa Israel wamesema, unalenga kuisadia nchi hiyo kufanikisha malengo yake ya kivita ya kuwashinda Hamas na kuwakombowa mateka wanaoshikiliwa Gaza.