Israel yaendeleza mashambulizi yake katika ukanda wa Gaza
24 Machi 2025Wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza imesema mashambulizi yaliyofanywa na Israel usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Nasser iliyopo katika eneo la Khan Yunis kusini mwa ukanda huo yamesababisha vifo vya watu wawili, na wengine wamejeruhiwa na yamesababisha moto mkubwa.Watu wawili wauwawa Gaza, mmoja achomwa kisu Israel
Kwa mujibu wa wizara hiyo ya afya iliyo chini ya Hamas, waliouawa katika shambulio hilo ni pamoja na mvulana wa miaka 16 ambaye alifanyiwa upasuaji siku mbili zilizopita na Ismail Barhoum, ambaye ni mwanachama Hamas ambaye alikuwa anatibiwa hospitalini hapo.
Jeshi la Israel limesema limefanya shambulio hilo katika hospitali ya Nasser likiwalenga wanamgambo wa Hamas wanaoendesha shughuli zao katika hospitali hiyo na kuilaumu Hamas kwa mauaji ya raia kwa kuendesha shughuli zake katika maeneo yenye watu wengi.
Hadi sasa zaidi ya Wapalestina 50,000 sasa wameuawa katika vita hivyo vya miezi 17 kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza.