SiasaIsrael
Israel yaendelea kutanua opereshi zake Gaza
4 Aprili 2025Matangazo
Katika taarifa yake, jeshi hilo limesema limefanya mashambulizi katika eneo la Shejaiya, ambako linadai limewauwa wanamgambo wa Hamas na kuharibu miundombinu yao. Hata hivyo haikutoa idani ya majeruhi.
Soma pia: Israel yatangaza kutanua mashambulizi ya ardhini kaskazini mwa Ukanda wa Gaza
Waziri wa Ulinzi Israel Katz awali alitangaza kwamba wamepiga hatua kubwa katika uwanja wa mapambano katika kile alichokitaja kama "kusafisha eneo la magaidi na miundombinu ya ugaidi."
Kartz amedokeza pia jeshi la Israel limefanikiwa kuchukuwa udhibiti wa maeneo muhimu na kusogeza operesheni zake kusini mwa Ukanda wa Gaza.