Israel yaendelea kushambulia Gaza, 11 wauawa
13 Agosti 2025Aidha, Wizara ya Afya imesema watu wengine watano wameripotiwa kufa huko Gaza kutokana na utapiamlo, na hivyo kupelekea idadi ya waliokufa njaa hadi sasa kufikia watu 227.
Wakati Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akitetea hapo jana wazo lake la kuwahamisha Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza , Kiongozi wa Hamas Khalil Al-Hayya amewasili mjini Cairo kwa mazungumzo ya kutafuta namna ya kufufua mpango wa amani unaoungwa mkono na Marekani unaohusisha usitishwaji mapigano kwa siku 60 na kuachiliwa kwa mateka.
Hayo ni baada ya duru ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Israel na Hamas kumalizika huko Qatar mwishoni mwa mwezi uliopita bila mafanikio yoyote. Na sasa Israel imesema inatarajia kutanua operesheni zake za kijeshi ili kuudhibiti mji wa Gaza, hatua inayokosolewa vikali kimataifa.