MigogoroMashariki ya Kati
Watu 25 wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel
30 Juni 2025Matangazo
Israel imewaamuru pia siku ya Jumatatu raia kuondoka katika maeneo hayo, kama ishara kuwa operesheni hiyo itaendelea.
Hayo yanajiri wakati hapo jana, rais wa Marekani Donald Trump alitoa wito wa kusitisha vita hivyo vilivyodumu kwa miezi 20.
Washauri wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wanatarajiwa kusafiri kuelekea mjini Washington kushiriki mazungumzo kuhusu mizozo ya Gaza na Iran, pamoja na uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano mapana ya kidiplomasia katika kanda hiyo ya Mashariki ya Kati.