Israel yadaiwa kuwashambulia watu wanaopokea misaada Gaza
27 Juni 2025Misaada hiyo ilikuwa inatolewa na polisi wa Palestina waliopata misaada hiyo kutoka kwa wahalifu waliyoipora kutoka kwa magari ya misaada ya kiutu.
Shambulizi hilo ni la hivi karibuni, linalohusisha watu kushambuliwa wakati wanapopokea misaada ya chakula. Baada ya kuzuwia chakula kuingia katika eneo hilo la Gaza, Israel imekubali malori machache ya misaada hiyo kuingia huko tangu mwezi Mei.
Juhudi za Umoja wa Mataifa kusambaza chakula hazijafua dafu kutokana na changamoto ya kuwepo wahalifu waliojihami wanaoiba chakula.
Watu wasiopungua 35 wameuawa katika mashambulizi yaUkanda wa Gaza
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi wa taifa hilo Israel Katz kwa pamoja wameishutumu Hamas kuiba chakula kunachoingia Kaskazini mwa Gaza na kutoa wito kwa jeshi la Israel kuzuwia hilo.