Israel yaapa kuishushia Gaza kuilazimisha Hamas ijisalimishe
8 Septemba 2025Matangazo
Haya yanajiri wakati Rais Donald Trump wa Marekani akisisitiza pendekezo jipya la usitishaji mapigano.
Mashambulizi mapya yamewaua takribani Wapalestina 40, wakiwemo mwandishi habari na watoto, na kusababisha maafa zaidi katika Ukanda huo, ambako tayari zaidi ya watu 64,000 wameshauawa tangu vita kuanza Oktoba 7 mwaka 2023.
Hata hivyo Hamas imesema iko tayari kuwaachia mateka, iwapo vita vitasitishwa na vikosi vya Israel kuondoka. Israel nayo inasisitiza haitakomesha operesheni zake hadi Hamas ikabidhi silaha zake.